Thursday, April 13, 2017

UEFA YAKANUSHA KUPUUZA TAARIFA ZA KUTAKIWA KUSOGEZA MBELE MCHEZO WA DORTMUND NA MONACO.

SHIRIKISHO la Soka la Ulaya-UEFA limejibu tuhuma za kushindwa kuahirisha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Borussia Dortmund dhidi ya Monaco, ba kusisitiza hawakupata taarifa zozote kuwa timu hizo hazikutana kucheza. Mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali uliahirishwa Jumanne baada ya basi la timu ya Dortmund kushambuliwa na milipuko wakati wakitoka hotelini kuelekea Signal Iduna Park. Mchezo huo ulikuja kuchezwa jana, lakini meneja wa Dortmund Thomas Tuchel alikuwa akihitaji muda zaidi ili wale waliokumbwa na tukio hilo waweze kusahau lakini alipuuziwa. Naye meneja wa Monaco Leonardo Jardim amekiri ilikuwa vigumu kwa wachezaji kuwa mchezoni baada ya timu yake kupata ushindi wa mabao 3-2 kwenye mchezo wao wa jana. Msemaji wa UEFA, amesema uamuzi wa kusogeza mbele mchezo wa Dortmund na Monaco uliamuliwa kwa kushirikisha pande zote mbili. UEFA iliendelea kudai kuwa ilikutana na pande zote mbili na kamwe hawakupewa taarifa yeyote ya kusogeza mbele zaidi mchezo huo.

No comments:

Post a Comment