Thursday, April 13, 2017

DYBALA ASAINI MKATABA MPYA JUVENTUS.

MSHAMBULIAJI wa Juventus, Paulo Dybala amesaini mkataba mpya na mabingwa hao wa Italia ambao utamalizika mwaka 2022. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 23 amefunga mabao 16 kwa Juventus msimu huu na kulikuwa na tetesi zikimuhusisha na kuondoka. Dybala alijiunga Juventus kwa kitita cha paundi milioni 23 kutoka Palermo na kupewa mkataba wa miaka mitano Juni 2015 na kufanikiwa kushinda mataji mawili mwaka jana. Dybala amesema siku zote amekuwa akitaka kufanikiwa kwenye kila kitu na anafahamu Juventus ndio mahali sahihi kuwepo kama anataka kushinda mataji. Dybala amefunga mabao 39 na kusaidia mengine 16 kwenye mechi 82 toka ajiunge na Juventus, ikiwa ni dadi kubwa zaidi ya mchezaji yeyote katika klabu kwa muda aliojiunga.

No comments:

Post a Comment