Friday, April 14, 2017

MOURINHO ATUPA LAWAMA KWA BEKI ZAKE.

MENEJA wa Manchester United, Jose Mourinho amewalaumu washambuliaji wa kikosi chake kwa kukosa umakini baada ya Anderlecht kusawazisha dakika za mwisho na kupata sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Europa League. United walikuwa wakiongoza kwa bao 1-0 dhidi ya timu hiyo ya Ubelgiji mpaka dakika ya 86, wakati wenyeji hao waliposawazisha kwa shuti lao la kwanza lililolenga lango la United. Akizungumza na wanahabari, Mourinho amesema kama angekuwa beki wa United ni wazi angekuwa amekasirika na washambuliaji walivyofanya. Mourinho aliendelea kudai kuwa mabeki walifanya kazi nzuri lakini watu waliostahili kumaliza mchezo walishindwa kufanya hivyo pamoja nafasi nyingi walizopata.

No comments:

Post a Comment