MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema hakuwa kufikiria kuwa siku moja angeweza kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 100 kwenye michuano ya Ulaya wakati anaanza, lakini anaona fahari na furaha kufikia mafanikio hayo. Ronaldo mwenye umri wa miaka 32 alifikia idadi hiyo baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 2-1 waliopata Madrid dhidi ya Bayern Munich juzi kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza war obo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno alitunukiwa shati maalumu la kumbukumbu na rais wa Madrid Florentino Perez jana kufuatia mafanikio hayo aliyopata. Akikaririwa na tovuti ya klabu hiyo, Ronaldo amesema ni heshima kubwa kufikisha idadi ya mabao 100 Ulaya na juzi ilikuwa ni siku maalumu na ushindi muhimu. Ronaldo aliendelea kwa kuishukuru klabu kwa nafasi ya kipekee waliyompa, wachezaji wenzake na mashabiki kwa kumuunga mkono. Ronaldo alianza kufunga mabao Ulaya katika mchezo kati ya Manchester United dhidi ya Debrecen Agosti mwaka 2005.
No comments:
Post a Comment