KIUNGO wa Arsenal, Mesut Ozil amedai kuwa hataki mazungumzo ya mkataba yakabugudhi kipindi hiki muhimu kuelekea mwishoni mwa msimu na anatarajia kusubiri mpaka Ligi Kuu itakapomalizika kabla ya kuzungumza mustakabali wake. Nafasi ya Ozil katika klabu hiyo limekuwa jambo jambo linalojadiliwa na vyombo vya habari nchini Uingereza huku taarifa zikidai nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 ambaye mkataba wake umebakiza chini ya kiezi 15, amekataa kusaini mkataba mpta utakaomuwezesha kupata paundi 250,000 kwa wiki. Arsenal kwasasa wanashikilia nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi wakiwa alama saba nyuma ya nafasi nne za juu. Akizungumza na wanahabari kuhusiana na hilo, Ozil amesema kwa kipindi hiki yeye sio muhimu sana kwani klabu ndio muhimu zaidi. Ozil aliendelea kudai kuwa bado wana kibarua kizito msimu huu hivyo anadhani sio sahihi kufikiria jambo linguine zaidi ya soka.
No comments:
Post a Comment