Friday, April 14, 2017

PIGO BAYERN, BOATENG, HUMMELS PANCHA.

MABEKI wa Bayern Munich Jerome Boateng na Mats Hummels wameondolewa katika mchezo wa Bundesliga dhidi ya Bayer ya Bayer Leverkusen unaotarajiwa kuchezwa kesho. Hummels alipata matatizo ya kifundo cha mguu na kumfanya kukosa mchezo wa robo fainali ya mkondo wa kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo walifungwa mabao 2-1 na Real Madrid juzi. Meneja wa Bayern ameithibitisha kuwa Boateng anasumbuliwa na tatizo la misuli na anatarajia kutomtumia mwishoni mwa wiki hii, ingawa ana matumaini atakuwa tayri kwa ajili ya mchezo dhidi ya Madrid wiki ijayo. Akizungumza na wanahabari, Ancelotti alithibitisha taarifa hizo za kuwakosa nyota wake hao kesho na kubainisha kuwa atawatumia David Alaba katikati na Juan Bernat upande wa kushoto wa safu yake ya ulinzi.

No comments:

Post a Comment