Wednesday, April 12, 2017

MARC BARTA ATUMA UJUMBE KUWASHUKURU MASHABIKI.

BEKI wa Borussia Dortmund, Marc Barta ametuma ujumbe wa kushukuru katika kurasa zake za mitandao ya kijamii za Instagram na Twitter kufuatia shambulio la kigaidi katika basi lao jana. Milipuko mitatu ilitokea karibu na basi la Dortmund lililokuwa njiani kuelekea katika mchezo wao wa robo fainali ya mkondo wa kwanza wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Monaco katika Uwanja wa Signal Idun Park. Mlipuko mmoja ulivunja vioo vya basi hilo na kumuumiza Barta ambaye alifanyiwa upasuaji wa kiganja jana usiku. Beki huyo alituma ujumbe katika Instagram na Twitter leo akidai kuwa anaendelea vyema na kuwashukuru mashabiki kwa salamu zao za pole.

No comments:

Post a Comment