Wednesday, April 12, 2017

MMOJA AKAMATWA TUKIO LA DORTMUND.


POLISI nchini Ujerumani inamshikilia mtuhumiwa mmoja anayehusishwa na kundi la Waislamu wenye msimamo mkali kufuatia shambulio la bomu katika basi la timu ya Borussia Dortmund. Waendesha mashitaka pia wamesema moja kati ya milipuko iliyotumika katika shambulio la jana ni ilikuwa na vipande vya chuma. Barua mbili zinadai kuhusika na shambulio hilo nazo zinachunguzwa. Waendesha mashitaka hao wanalichukulia tukio hilo kama la shambulio la kigaidi lakini wamesema hawaelewi lengo lake haswa lilikuwa ni nini. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel mapema jana leo amesema shambulio hilo ni uhalifu wa kutisha na kuwapongeza mashabiki wa timu zote mbili kwa kuungana.

No comments:

Post a Comment