Wednesday, April 12, 2017

BAYERN HATIHATI KUMKOSA LEWANDOWSKI LEO.

KLABU ya Bayern Munich inatarajiwa kumkosa mshambuliaji wake mahiri Robert Lewandowski kwa ajili ya mchezo wao war obo fainali ya mkondo wa kwanza wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya nyumbani dhidi ya Real Madrid baadae leo. Lewandowski ambaye amefunga mabao 38 katika mechi 40 alizoichezea timu hiyo msimu huu, kuna hatihati akakosa mchezo huo baada ya kuumia bega Jumapili iliyopita. Hata hivyo, meneja wa Bayern Carlo Ancelotti ambaye aliiongoza Madrid kutwaa taji lake la 10 la Ulaya mwaka 2014 amesema kikosi chake bado kinaweza kuwa imara bila nyota huyo. Akizungumza na wanahabari, Ancelotti amesema kama Lewandowski atakuwa katika maumivu hatacheza lakini haiweza kubadili mipango yao.

No comments:

Post a Comment