Wednesday, April 12, 2017

UEFA KUIMARISHA ULINZI MECHI ZALEO.

SHIRIKISHO la Soka la Ulaya-UEFA linafuatilia masuala ya kiusalama kwa ajili ya mechi za robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya zitakazochezwa baadae leo, baada ya shambulio lililolenga basi la timu ya Borussia Dortmund. Basi hilo liliharibiwa na milipuko mitatu iliyotokea wakati klabu hiyo ikiwa njiani kutoka hotelini kuelekea Signal Iduna Park jana kwa ajili ya mchezo wao wa mkondo wa kwanza dhidi ya Monaco. Polisi hawakuweza kugundua aina ya mlipuko uliotumika lakini wameelezea kuwa ulikuwa mbaya na kuongeza kuwa wanaendelea kufanya uchunguzi ili kugundua kama ni shambulio la kupangwa. Kufuatia tukio hilo, UEFA imeamua kuimarisha ulinzi zaidi katika mechi tatu zitakazopigwa le ukiwemo ule wa Atletico Madrid dhidi ya Leicester City, Real Madrid dhidi ya Bayern Munich na ule ulioahirishwa wa Dortmund dhidi ya Monaco. Katika taarifa yake UEFA ilidai kuwa hakuna taarifa zozote za tishio kwa mechi za leo na kuwahakikishia mashabiki, wachezaji na viongozi kuwa wanafanya kila wawezalo juu ya usalama wa mechi hizo.

No comments:

Post a Comment