Wednesday, April 12, 2017

MKHITARYAN ATUMA SALAMU ZA POLE KWA DORTMUND.

KIUNGO wa Manchester United, Henrikh Mkhitaryan ametuma salamu za pole klabu yake ya zamani wa Borussia Dortmund baada ya basi walilokuwa wakisafiria kulipuliwa na milipuko mitatu. Wachezaji na baadhi ya viongozi wa klabu walikuwa wakisafiri kwenda Signal Iduna Park kwa ajili ya mchezo wao wa mkondo wa kwanza wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Monaco wakati basi liliposhambuliwa. Beki wa kati wa Dortmund Marc Barta aliumia kiganja cha mkono wake kwenye tukio na kukimbizwa hospitali ambapo alifanyiwa upasuaji mdogo na sasa anaendelea vyema. Mkhitaryan ambaye aliichezea mechi 140 Dortmund kwa misimu mitatu naye pia alitumia mtandao wake wa kijamii kuonyesha kuiunga mkono klabu hiyo. Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Mkhitaryan alieleza kusikitishwa na kushtushwa na mlipuko huo na kuwatakia viongozi, wachezaji na mashabiki pole.

No comments:

Post a Comment