Wednesday, April 12, 2017

SIJAWAHI KUWA NA MGOGORO NA RANIERI - SHAKESPEARE.

MENEJA wa Leicester City, Craig Shakespeare amesema kamwe hakuwa na mgogoro na meneja wa zamani Claudio Ranieri. Ranieri alitimuliwa na mabingwa hao wa Ligi Kuu Februari na Jumatatu usiku alidai kuwa kuna mtu nyuma yake alifanya isivyo sawa juu yake. Shakespeare amesema kamwe hakuwahi kuwa na ugomvi wowote wala kupishana kauli na Ranieri. Ranieri alidokeza kuwa kuna mtu alimhujumu wakati akiwa Leicester lakini alikataa kutaja jina lolote hatua ambayo ilizua tetesi za kumhusisha Shakespeare aliyekuwa msaidizi wake.

No comments:

Post a Comment