Wednesday, April 12, 2017

DORTMUND KUIKABILI MONACO PAMOJA NA TAHARUKI.

WACHEZAJI wa kikosi cha Borussia Dortmund waliopo katika mshtuko watalazimika kusahau tukio lililowatokea kwa muda wakati wakapokwaana na Monaco katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baadae leo. Mchezo huo unachezwa saa 24 baada ya kuahirishwa kufuatia mlipuko uliotokea kwenye basi lao wakati wakielekea katika Uwanja wa Signal Iguna Park kutoka hotelini kwao. Beki Marc Barta alipata majeruhi ya kiganja cha mkono kwenye tukio hilo. Ofisa mkuu wa Dortmund Hans-Joachim Watzke amesema katika tukio kama hilo wachezaji wote wanapaswa kujikusanya na kusahau kwa muda tukio hilo kwa ajili ya mchezo ulio mbele yao. Watzke aliendelea kudai kuwa anafahamu wachezaji na makocha wote wako kwenye mshtuko hivyo sasa wanapaswa kutafuta njia mbadala.

No comments:

Post a Comment