Tuesday, April 11, 2017

MAREKANI, CANADA, MEXICO WAOMBA KUANDAA KWA PAMOJA KOMBE LA DUNIA 2026.

MAREKANI, Canada na Mexico zimetangaza kuomba kwa pamoja zabuni ya kuwa wenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia 2026. Hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa michuano hiyo baada ya kuongezwa kutoka timu 32 mpaka 48 na kama ikifanikiwa itakuwa mara ya kwanza kwa Kombe la Dunia kuandaliwa na nchi tatu. Maombi yanatarajiwa kuwa Marekani itakuwa mwenyeji kwa mechi 60, huku mechi 10 zitakazosalia watagawana Canada na Mexico. Uamuzi wa nani atakuwa mwenyeji wa michuano hiyo unatarajiwa kutangazwa mwaka 2020. Marekani imewahi kuandaa michuano hiyo mwaka 1994 ambayo ndio iliyohudhuriwa na watu wengi zaidi katika historia ya michuano hiyo, wakati Mexico ndio taifa la kwanza kuandaa michuano hiyo mara mbili mwaka 1970 na 1986, huku Canada wao michuano yao mikubwa kuandaa ikiwa ni Kombe la Dunia la wanawake mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment