Thursday, April 6, 2017

"NIPO FITI" - LEWANDOWSKI AWATOA HOFU MASHABIKI WA BAYERN.

MSHAMBULIAJI nyota wa Bayern Munich, Roberto Lewandowski amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kufuatia majeruhi aliyopata wakati wa mazoezi. Mapema leo Lewandowski alipigwa picha akiwa mazoezini ameshikilia msuli wa paja kwa hisia za maumivu hivyo kuzua wasiwasi kama atakuwepo kwenye mchezo muhimu wa Jumamosi hii wa Bundesliga dhidi ya Borussia Dortmund. Baadhi ya vyombo vya habari nchini Ujerumani vilikuwa vimeripoti kuwa Lewandowski amechanika msuli wa paja na anaweza kukaa kwa muda nje ya uwanja. Hata hivyo, nyota huyo aliibuka na kukanusha taarifa hizo zilizozagaa huku akiwaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuwa anasikia vyema na yuko fiti. Bayern mbali na kukabiliwa na mchezo dhidi ya Dortmund kwenye Bundesliga Jumamosi hii, pia wanakabiliwa na mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment