Thursday, April 6, 2017

OZIL AMFURAHISHA WENGER.MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema Mesut Ozil amefanikiwa kusahau kuondolewa kwao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na sasa amehamishia nguvu zake katika Ligi Kuu. Kauli hiyo ya Wenger imekuja kufuatia ushindi mnono wa mabao 3-0 waliopata dhidi ya West Ham United jana na kuwapandisha mpaka nafasi ya tano kutoka ile ya sita. Katika miezi ya karibuni Ozil alionekana kuwa chini ya kiwango lakini jana alionyesha kiwango kikubwa kwa kufunga bao moja na kutengeneza linguine katika ushindi wa pili wa Arsenal kati ya mechi saba za ligi zilizopita. Akizungumza na wanahabari, Wenger amesema anadhani Ozil amerejea kwenye ubora wake kwani anamfahamu vyema. Wenger aliendelea kudai kuwa anadhani kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kulimuathiri kwa kiasi kikubwa na ilimchukua muda kusahau.

No comments:

Post a Comment