Thursday, April 6, 2017

CONTE SASA AUONA UBINGWA UKIKARIBIA.MENEJA wa Chelsea Antonio Conte amesema kikosi chake kimepiga hatua kubwa kuukaribia ubingwa wa Ligi Kuu baada ya ushindi wa mabao 2-1 waliopata dhidi ya Manchester City jana kwenye Uwanja wa Stamford Bridge. Eden Hazard alifunga mabao mawili katika kipindi cha kwanza huku Sergio Aguero akifunga la kusawazisha la City, wakati Chelsea wakirejesha makali yao ya ushindi kufuatia kipigo cha mabao 2-1 walichopata nyumbani kutoka kwa Crystal Palace. Ushindi huo unaifanya Chelsea kuendelea kujiimarisha kileleni kwa tofauti ya alama saba dhidi ya Tottenham Hotspurs wanaoshikilia nafasi ya pili huku kukiwa kumebaki mechi nane msimu kumalizika. Akizungumza na wanahabari, Conte amesema ushindi huo ni hatua kubwa dhidi ya timu kubwa. Conte aliendelea kudai kuwa kushinda mchezo mgumu baada ya kutoka kufungwa sio jambo jepesi na anashukuru wachezaji wake wameonyesha ubora wao.

No comments:

Post a Comment