Thursday, April 6, 2017

BROOS KUENDELEA KUBAKI CAMEROON.

KOCHA wa timu ya taifa ya Cameroon, Hugo Broos amesisitiza anataka kuendelea kubaki na kibarua chake ikiwa imepita wiki moja baada ya kudai anafikiria kuhusu mustakabali wake. Kocha huyo raia wa Ubelgiji alitishia kujiuzulu kufuatia matatizo ya kiongozi na fedha lakini baada ya kukutana na viongozi wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo amebadili uamuzi wake. Broos pia amekanusha tetesi kuwa aliomba kibarua cha kwenda kuinoa timu ya taifa ya Ghana maarufu kama Black Stars, ambao wamemteua Kwesi Appiah kushika nafasi hiyo. Broos mwenye umri wa miaka 64 amesema hataki kuondoka Cameroon kwnai kama angetaka kuondoka angeshafanya hivyo kitambo.

No comments:

Post a Comment