Thursday, April 6, 2017

DORTMUND YAMLIMA FAINI AUBAMEYANG.

KLABU ya Borussia Dortmund imemlima faini Pierre-Emerick Aubameyang kufuatia kushangilia huku akiwa amevaa kinyago kwenye sare ya bao 1-1 waliyopata dhidi ya Schalke Jumamosi iliyopita. Aubameyang mwenye umri wa miaka 27 alifunga bao la kuongoza kwenye mchezo huo na kuanza kushangilia huku akiwa amevaa kinyago ambacho baadae iligundulika kuwa sehemu ya kampeni ya Nike ambao wanamdhamini. Hiyo inakuwa mara ya pili kwa Aubameyang ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuwatangaza wadhamini wake hao wakati akiichezea Dortmund ambao wanadhaminiwa na kampuni ya vifaa vya michezo ya Puma. Katika taarifa yake Dortmund wamedai kuwa walifanya mazungumzo na Aubameyang baada ya mchezo wa Juzi ambao walishinda mabao 3-0 dhidi ya Humburg huku nyota huyo wa kimataifa wa Gabon akifunga bao moja na kusaidia lingine.

No comments:

Post a Comment