Wednesday, April 26, 2017

RONALDO KUIKOSA DEPORTIVO.

MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameachwa katika kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mchezo wao wa La Liga dhidi ya Deportivo La Coruna. Meneja wa Madrid, Zinedine Zidane ametaja kikosi cha wachezaji 19 kwa ajili ya mchezo huo huku Gareth Bale pia akiondolewa kutokana na majeruhi. Bale alipata majeruhi mwishoni mwa wiki iliyopita na anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki tatu. Huku Ronaldo na Bale wakikosekana, kuna uwezekano mkubwa kwa Zidane kuwatumia Karim benzema na Alvaro Morata katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo. Beki Sergio Ramos naye anatarajia kukosa mchezo huo utakaochezwa baadae leo akitumikia adhabu ya kukosa mechi moja baada ya kupewa kadi nyekundu katika mchezo wa El Clasico dhidi ya mahasimu wao Barcelona Jumapili iliyopita.

No comments:

Post a Comment