Tuesday, April 25, 2017

WENGER ASISITIZA GIROUD HAENDI POPOTE.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amepuuzia tetesi kuwa nyota wa kimataifa wa Ufaransa Olivier Giroud anaweza kuondoka katika klabu hiyo na kwenda Olympique Marseille mwishoni mwa msimu huu. Taarifa kutoka nchini Ufaransa zimedai kuwa Rudi Garcia alikuwa anataka kumrejesha Giroud nchini humo na walikuwa wamejipanga kutuma ofa Arsenal. Hata hivyo, Wenger amesisitiza kuwa mpaka sasa hajapata taarifa zozote kutoka katika klabu hiyo kuhusiana na suala hilo. Akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Leicester City, Wenger amesema bado hajafuatwa na Marseille kuhusiana na suala hilo na kuongeza kuwa bado wanataka kuendelea kubakia na Giroud. Giroud alijiunga na Arsenal akitokea Montpellier mwaka 2012 na toka wakati huo ameshacheza mechi zaidi ya 200 na mkataba wake unatarajiwa kumalizika Juni mwaka 2019.

No comments:

Post a Comment