Tuesday, April 25, 2017

WAKALA WA GRIEZMANN ATHIBITISHA NIA YA MAN UNITED KUMUWINDA NYOTA HUYO.

WAKALA wa mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann amesema Manchester United wameonyesha nia ya kumsajili nyota huyo. United ambao wanashikilia nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu, wamekuwa wakifunga mabao kadhaa dhidi ya timu zinazoshikilia nafasi sita za juu katika msimamo na bado wanataka kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji kwa kumsajili Griezmann ambaye ameifungia Atletico mabao 25 msimu huu. Wakala huyo, Eric Olhats amesema kwasasa wako katika mpango wa kutafuta taarifa kutoka katika klabu ambazo zinataka kumsajili mteja wake huyo. Olhats aliendelea kudai kuwa kitenzi katika mkataba wa Griezmann ni euro milioni 100 hivyo kuna timu chache zilizoonyesha nia ikiwemo United, Manchester City, Chelsea, Barcelona na Real Madrid. Hata hivyo, Olhats amesema United ndio wamekuwa wa kwanza kuwafuata kuhusiana na suala hilo mpaka sasa.

No comments:

Post a Comment