Tuesday, April 25, 2017

CONTE AZING'ONG'A KLABU ZA MANCHESTER.

MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte amesema kutumia fedha nyingi kwa ajili ya wachezaji hakukupi uhakika wa mafanikio katika Ligi Kuu ya Uingereza. Meneja huyo raia wa Italia ametolea mfano klabu za Manchester baada ya Manchester United kutumia kiasi kilichovunja rekodi cha paundi milioni 89 kwa ajili ya kiungo Paul Pogba na Manchester City wakitumia paundi milioni 47 kwa beki John Stones. Chelsea wako kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama nne dhidi ya Tottenham Hotspurs wanaoshika nafasi pili huku pia wakitofautiana alama 11 na City na 12 kwa United zikiwa zimebaki mechi sita ligi kumalizika. Akizungumza na wanahabari, Conte amesema ni muhimu kuelewa kuwa sio mara zote wanaotumia fedha nyingi kwenye usajili hushinda. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa msimu huu sio pekee klabu za Manchester kutumia fedha nyingi katika usajili, lakini mafanikio hayategemei fedha pekee.

No comments:

Post a Comment