Tuesday, April 25, 2017

MARTIN ATKINSON KUCHEZESHA MANCHESTER DERBY.

LIGI Kuu ya Uingereza imethibitisha mwamuzi Martin Atkinson ndio aliyechaguliwa kuchezesha mchezo wa Manchester derdy kesho kutwa. Atkinson mwenye umri wa miaka 46 anatarajiwa kuwa mwamuzi kiongozi wakati Manchester United itakapowafuata majirani zao Manchester City katika Uwanja wa Etihad.  Mwamuzi huyo kutoka West Yorkshire ameshachezesha mechi tatu za United msimu huu ikiwemo waliyofungwa mabao 4-0 na Chelsea Octoba 23 na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Sunderland Desemba 26 pamoja na ile ya Kombe la FA dhidi ya Blackburn Rovers Februari 19. Kwa upande wa City, Atkinson ameshachezesha mechi mbili ikiwemo ile waliyoshinda mabao 2-1 dhidi ya Arsenal Desemba 18 pamoja na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sunderland Machi 5 mwaka huu. Atkinson pia aliwahi kuchezesha derby ambayo United walishinda katika msimu wa 2009-2010.

No comments:

Post a Comment