Tuesday, April 25, 2017

BARCELONA YAWEKA WAZI KUWA HAWANA MPANGO WA KUMUUZA NEYMAR.

KATIBU wa ufundi wa Barcelona, Roberto Fernandez ameondoa uwezekano wa kumuuza nyota wao Neymar huku apuuzia tetesi kuwa wana mpango wa kumsajili nyota wa Juventus Paul Dybala. Neymar mwenye umri wa miaka 25 amekuwa akihusishwa na tetesi kwa kipindi kirefu za kwenda kwa wakongwe wa Ligi Kuu Manchester United. Lakini Fernandez amesema hakuna nafasi kwa Neymar ambaye ana mkataba unaomalizika katikati ya 2021, kuondoka Camp Nou. Akizungumza na wanahabari kuhusiana na suala hilo, Fernandez amesema Neymar hauziki na kuongeza kuwa klabu zinazomuwani zinajisumbua kwasasa. Akizungumzia suala la Dybala, Fernandez amesema ni mchezaji mzuri lakini tayari Barcelona ina safu bora kabisa ya ushambuliaji hivyo hadhani kama uhamisho huo utawezekana.

No comments:

Post a Comment