Thursday, May 11, 2017

CONTE ASISITIZA KUBAKI CHELSEA.

MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte amesisitiza anataka kuendelea kuinoa Chelsea kwa kipindi kirefu kijacho pamoja na tetesi mpya zinazomuhusishwa na kwenda kuinoa Inter Milan. Meneja huyo raia wa Italia amebakisha ushindi katrika mechi moja pekee ili aweze kuisaidia Chelsea kutwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza katika msimu wake wa kwanza Stamford Bridge. Chelsea wanaweza kufanikiwa kushinda taji hilo kama wakifanikiwa kuifunga West Bromwich Albion Ijumaa hii katika Uwanja wa The Hawthorns. Hata hivyo, mapema msimu huu meneja huyo wa zamani wa Juventus alikuwa akihusishwa na tetesi za kurejea nchini Italia kwa kuwa kocha wa Inter kufuatia klabu hiyo kumtimua Stefano Pioli. Akiulizwa kuhusiana na suala hilo, Conte amesema bado ana mkataba wa miaka miwili na Chelsea na anataka kuendelea kubakia hapo mpaka mkataba wake utakapomalizika.

No comments:

Post a Comment