Thursday, May 11, 2017

VALENCIA YAPATA KOCHA MPYA.

KLABU ya Valencia, imethibitisha kumteua Marcelino kuwa kocha wa mpya kwa ajili ya msimu ujap wa La Liga. Valencia wamekuwa na msimu mbaya La Liga mpaka kuingia katika mtikisiko wa kushuka daraja chini ya Pako Ayestaran kabla ya kutimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Cesare Prandelli ambaye naye alijiuzulu Desemba mwaka jana baada ya kutoelewana na bodi juu ya masuala ya usajili. Voro alichukua mikoba ya Prandelli na kufanikiwa kuiondoa Valencia kutoka katika hatari ya kushuka daraja mpaka nafasi ya 13 katika msimamo wa La Liga. Voro anatarajiwa kuendelea kuinoa Valencia katika michezo yao miwili iliyosalia msimu huu kabla ya Marceilino kukabidhiwa rasmi kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao.

No comments:

Post a Comment