Thursday, May 11, 2017

THIERRY HENRY KUMBE SHABIKI WA KUTUPWA WA SPURS.

NGULI wa soka wa zamani wa Ufaransa, Thierry Henry ataendelea siku zote kukumbwa na Arsenal kama mfungaji bora wa wakati wote lakini mwenyewe amekiri kuwa mshabiki mkubwa wa timu ya San Antonio Spurs inayoshiriki Ligi ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani-NBA. Henry aliweka rekodi Arsenal ya kufunga jumla ya mabao 228 katika vipindi viwili tofauti alivyoichezea timu hiyo. Umahiri wake huo katika kufunga mabao umemfanya kutengenezewa sanamu lake nje ya Uwanja wa Emirates na anatajwa kuwa mmoja kati ya wachezaji bora kabisa kuwhai kutokea katika Ligi Kuu ya Uingereza. Hata hivyo, Henry ambaye kwasasa anafurahi maisha ya kustaafu, ameonekana katika mechi za mtoano za NBA katika jiji la San Antonio ambapo Spurs walikuwa wkaipepetana na Houston Rockets. Katika mchezo huo Henry alishuhudia timu yake pendwa na Spurs ikiibuka na ushindi wa vikapu 110-107 na kuwafanya kuongoza kwa michezo 3-2 kati ya saba ambayo watacheza kwenye hatua hiyo ya mtoano.

No comments:

Post a Comment