Thursday, May 11, 2017

MAMADOU SAKHO KUKOSA MECHI ZOTE ZILIZOSALIA ZA PALACE.

MENEJA wa Crystal Palace, Sam Allardyce amesema beki wake Mamadou Sakho hatarajiwi kucheza mechi mbili zilizobakia za Ligi Kuu msimu huu. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa, ambaye alijiunga na Palace kwa mkopo akitokea Liverpool Januari mwaka huu, amekuwa katika kiwango bora mpaka alipopata majeruhi ya goti katika mchezo waliofungwa bao 1-0 na Tottenham Hotspurs mwezi uliopita. Sakho alikosa michezo waliyopoteza dhidi ya Burnley na Manchester City na anatarajiwa pia kukosa mchezo muhimu dhidi ya Hull City Jumamosi hii. Allardyce pia amethibitisha kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 pia atakosa mchezo wao wa mwisho dhidi ya Manchester United utakaofanyika katika Uwanja wa Old Trafford.

No comments:

Post a Comment