Tuesday, May 9, 2017

ZIDANE KUIFUATA ATLETICO "FULL MZIKI"

MENEJA wa Real Madrid, Zinedine Zidane hatarajii kupunguza kasi yao wakati watakapowavaa mahasimu wao Atletico Madrid kesho. Madrid watakwenda katika mchezo huo wa marudiano wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaofanyika katika Uwanja wa Vicente Calderone wakiwa mbele kwa mabao 3-0 waliyopata katika mchezo wa mkondo wa kwanza. Klabu hiyo iko mbioni kutwaa mataji mawili ya La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini Zidane amekitaka kikosi chake kutobweteka kutokana na changamoto iliyopo mbele yao. Akizungumza na wanahabari, Zidane amesema wanakwenda katika mchezo huo kama wanavyofanya katika kila mchezo, kwa kuanza imara ili kujaribu kushinda hilo ndio lengo lao. Zidane aliendelea kudai kuwa hawatakwenda Vicente Calderone kuzuia, bali watakwenda kwa ajili ya kushambulia na kutafuta ushindi.

No comments:

Post a Comment