CHAMA cha Soka cha China-CFA kimekanusha kutoa kitita cha euro milioni 50 kwa ajili ya kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Loew ili aweze kwenda kuinoa timu ya taifa ya nchi hiyo. Vyombo vya habari nchini Hispania zimedai kuwa CFA walikuwa wamepanga kumchukua Loew kuwa kocha wao, ili aende kuziba nafasi ya kocha wa sasa Marcello Lippi. Hata hivyo, CFA bado wana imani kubwa na Lippi na hawana mpango wowote wa kumchukua Loew ambaye amekuwa na Ujerumani toka mwaka 2006. Lippi ameonekana kusuasua katika kampani yake ya kuiwezesha China kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi, hivyo kuzuka tetesi kuwa CFA inataka kumuondoa kocha huyo raia wa Italia. Katika taarifa yake, CFA wamesema taarifa kuhusu Loew hazina ukweli wowote kwani bado wana imani na Lippi kuendelea kuinoa timu hiyo.
No comments:
Post a Comment