Tuesday, May 9, 2017

WENGER AIDHIHAKI NAFASI YA UKURUGENZI WA MICHEZO.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amedhihaki nafasi ya Mkurugenzi wa Michezo na kusisitiza kuwa hawezi kufanya kazi na mtu wa aina hiyo Arsenal. Taarifa kutoka vyombo vya habari nchini Uingereza, vimekuwa vikimtaja mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Muchael Zorc kwenda Arsenal kupewa nafasi hiyo. Gazeti la The Daily Telegraph limedai kuwa klabu hiyo ya Ligi Kuu imezungumza na Zorc huku ikiaminika kuwa wanataka kumteua kushikilia nafasi hiyo mpya. Winga wa zamani wa Arsenal, Marc Overmars naye ametajwa kama mmoja wa watu wanaoweza kupewa nafasi hiyo lakini Wenger alipoulizwa kuhusiana na hilo alidhihaki akidai hajui kazi haswa ya watu hao. Wenger amesema hafahamu mkurugenzi wa michezo ina maana gani na kuongeza kuwa kama akiendelea kuwa meneja wa Arsenal yeye ndiye atakayeamua ni watu gani anaowahitaji kwenye benchi lake la ufundi.

No comments:

Post a Comment