Tuesday, May 9, 2017

CHELSEA INASTAHILI TAJI LA LIGI KUU - CONTE.

MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte amesema kikosi chake kinastahili kushinda taji la Ligi Kuu nchini Uingereza. Chelsea sasa wamebakisha ushindi katika mechi moja pekee ili waweze kutwaa taji lao la tano la ligi baada ya kuigaragaza Middlesbrough kwa mabao 3-0 katika Uwanja wa Stamford Bridge jana. Conte mwenye umri wa miaka 47, amesema msimu huu ni wa kwanza kwake nchini humo na yupo katika ligi ngumu. Akizungumza na wanahabari, Conte amesema amefurahishwa na wachezaji wake kwani wameonyesha wanastahili kushinda taji la ligi. Chelsea wanatarajiwa kupambana na West Bromwich Albion Ijumaa hii huku wakitofautiana alama saba na Tottenham Hotspurs ambao wanacheza na Manchester United Jumapili. Mabingwa hao watarajiwa watamaliza msimu kwa kucheza dhidi ya Watford na Suinderland ambao tayari wameshashuka daraja.

No comments:

Post a Comment