Tuesday, May 9, 2017

RAIS WA FIFA KUKUTANA NA SULLEY MUNTARI.

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Gianni Infantino amesema atazungumza na Sulley Muntari kufuatia mchezaji huyo wa Pescara kudai kufanyiwa vitendo vya kibaguzi katika mchezo wao wa hivi karibuni. Muntari mwenye umri wa miaka 32, ambaye alitolewa nje katika mchezo dhidi ya Cagliari Aprili 30 mwaka huu baada ya kuondoka uwanjani kupinga vitendo hivyo, anaamini kuwa FIFA na Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA hawachukui hatua stahiki kudhibiti vitendo hivyo. Infantino katika kampeni zake za kutafuta nafasi ya urais aliapa kupambana na watu wanaoedeleza vitendo vya kibaguzi. FIFA ilikosolewa kwa kutengua kikosi kazi cha kupambana na masuala ua ubanguzi wa rangi Septem,ba mwaka jana. Akiulizwa kuhusiana na suala hilo katika mkutano mkuu wa Shirikisho la Soka la Afrika-CAF uliofanyika huko Manama, Bahrain, amesema atazungumza na Muntari pamoja na rais wa Shirikisho la Soka la Italia-FIGC Carlo Tavecchio.

No comments:

Post a Comment