CHAMA cha Soka cha Uholanzi-KNVB kimethibitisha kumteua Dick Advocaat kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo. Kikosi cha Uholanzi kinachojulikana kama Orange kilikuwa hakina kocha kufuatia kutimuliwa kwa Danny Blind kulikotokana na kipigo kutoka kwa Bulgaria kwenye mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia iliochezwa machi mwaka huu. Advocaat ambaye anainoa nchi hiyo kwa mara ya tatu, ameteuliwa kushika nafasi hiyo mpaka mwishoni mwa kampeni za kufuzu Kombe la Dunia chini Urusi mwaka 2018 na mkataba wake utaongezwa kama akifanikiwa kuifikisha nchi hiyo kwenye fainali hizo. Nguli wa zamani wa soka wa nchi hiyo Ruud Gullit amechaguliwa kuwa kocha msaidizi na changamoto ya kwanza kwa Advocaat itakuwa ni kuinasua Uholanzi kutoka katika nafasi ya nne katika msimamo wa kundi A. Uholanzi kwasasa wana alama saba baada ya kucheza michezo mitano na wako nyuma ya vinara Ufaransa kwa alama sita kwenye kundi hilo.
No comments:
Post a Comment