Monday, May 8, 2017

RAIS WA CAF AKATAA MSHAHARA.

RAIS mpya wa Shirikisho la Soka la Afrika-CAF, Ahmad Ahmad amesema amekataa kulipwa mshahara na shirikisho hilo. Kuchaguliwa kwa Ahmad Machi mwaka huu, kulimaliza utawalaa wa Issa Hayatou wa Cameroon uliodumu kwa kipindi cha miaka 29. Akizungumza na wanahabari, Ahmad amesema amekataa kulipwa mshahara na CAF kwasababu haukidhi viwango vya utawala bora. Ahmad aliendelea kudai kuwa mishahara ya wafanyakazi wote wa CAF kuanzia watawala wa kamati ya utendaji na rais yote inapaswa kuwa ya wazi. Ahmad mwenye umri wa miaka 57 aliendelea kudai kuwa mfumo wa utawala ni jambo muhimu sana na kila mtu anapaswa kufahamu kitu gani kinaendelea.

No comments:

Post a Comment