Monday, May 8, 2017

LUKAKU AMWAGA 'POVU' KUHUSU TAARIFA ZA KUREJEA CHELSEA.

MSHAMBULIAJI wa Everton, Romelu Lukaku amepuuza taarifa zinazosambazwa na vyombo vya habari kuwa anaweza kurejea tena Chelsea. Jumapili usiku, Lukaku alituma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter akiwaambia waandishi wa habari waache kumfuatilia mambo yake ili aweze kutuliza akili Everton. Lukaku mwenye umri wa miaka 23 ambaye ana mkataba na Everton unaonalizika 2019, alikuwa ameripotiwa kukaa kusaini mkataba wa nyongeza hivyo kuzua tetesi anaweza kuondoka majira ya kiangazi. Chelsea ndio wanaotajwa kwa kiasi kikubwa na vyombo vya habari kuwa wanaweza kumnasa tena nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji. Tetesi hizo zimeonyesha kumuudhi Lukaku mwenyewe ambaye aliendelea kwa kuvitaka vyombo vya habari kuacha kuandika habari zake kama hajazithibitisha yeye mwenyewe.

No comments:

Post a Comment