Monday, May 8, 2017

N'GOLO KANTE ALAMBA TUZO NYINGINE.

KIUNGO wa Chelsea, N’Golo Kante ametuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka na Chama cha Waandishi wa Habari za Soka. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 ameisaidia Chelsea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu huku pia akiisaidia Leicester City kutwaa taji lao la kwanza la ligi msimu uliopita. Mapema mwezi uliopita Kante aliteuliwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Chama cha Wachezaji Bora wa Kulipwa-PFA huku pia akitajwa kwenye kikosi bora cha PFA kwa mwaka wa pili mfululizo. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amecheza mechi 33 za ligi akiwa na Chelsea msimu huu, huku akifunga bao moja na kusaidia lingine moja lakini msaada wake anaotoa kwenye safu ya ulinzi ndio uliomtengenezea sifa kubwa.

No comments:

Post a Comment