Monday, May 8, 2017

CHAPECOENSE YATWA TAJI LAKE LA KWANZA.

KLABU ya Chapecoense imefanikiwa kushinda taji lake la kwanza toka timu wachezaji wa timu hiyo walipofariki katika ajali ya ndege. Ni wachezaji watatu pekee wa klabu hiyo ya Brazil waliopona kwenye ajali iliyotokea Novemba mwaka jana ambapo watu 71 kati ya 77 walifariki dunia. Klabu kubwa kutoka Brazil na Argentina zilijitolea wachezaji wao kwa mkopo kwenda Chapecoense, ambao walisajili wachezaji wapya 25 na kuwapandisha wengine tisa kutoka timu ya vijana. Klabu hiyo imetwaa taji la ubingwa wa jimbo la Santa Catarina jana ikiwa ni mwaka wa pili mfululizo kufanya hivyo. Kocha mpya wa Chapecoense amesema ubingwa huo waliopata ni maalumu kwa ajili ya wachezaji na viongozi waliopoteza maisha kwenye ajali ya ndege.

No comments:

Post a Comment