Monday, May 8, 2017

SANCHEZ ASUBIRI MSIMU UMALIZIKE.

MSHAMBULIAJI nyota wa Arsenal, Alexis Sanchez amedai kuwa atajadili mustabali wake na meneja Arsene Wenger pindi msimu wa Ligi Kuu utakapofikia kikomo. Sanchez ambaye mkataba wake unamalizika Juni mwaka 2018, amekuwa akihusishwa na tetesi za kuondoka Emirates huku Bayern Munich ikitajwa kama moja ya klabu zinazomuwania. Akizungumza na wanahabari kuhusiana na mustakabali wake, Sanchez amesema kwasasa anataka kuweka nguvu zake katika kuisaidia timu kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na pia kutwaa taji la Kombe la FA. Sanchez aliendelea kudai kuwa msimu uatkapomalizika ndipo anaweza kukaa na Wenger na kuanza kujadili kuhusu mustakabali wake wa baadae.

No comments:

Post a Comment