Friday, May 5, 2017

MESSI ASHINDA RUFANI YAKE KUPINGA KUFUNGIWA MECHI NNE.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina, Lionel Messi yuko huru kuitumikia nchi yake katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia baada ya adhabu yake ya kufungiwa mechi nne kutenguliwa katika rufani. Nyota huyo wa Barcelona mwenye umri wa miaka 29, alifungiwa kufuatia kumtolea maneno machafu mwamuzi wa pembeni wakati wa mchezo ambao Argentina waliifunga Chile kwa bao 1-0 machi mwaka huu. Adhabu hiyo ilimfanya Messi kukosa mchezo mmoja wa kufuzu ambao Argentina walitandikwa mabao 2-0 na Bolivia. Kamati ya rufani ya FIFA imesema ingawa kitendo alichofanya hakikubaliki lakini hakuna ushahidi kamili kama nyota huyo alidhamiria kumtolea maneno hayo mwmauzi. Faini ya paundi 7,800 aliyotozwa Messi katika adhabu hiyo nayo pia imeondolewa.

No comments:

Post a Comment