Friday, May 5, 2017

GUARDIOLA KUWAKOSA AGUERO NA STONES.

MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Sergio Aguero na beki John Stones wanatarajiwa kukosa mchezo dhidi ya Crystal Palace utakaofanyika kesho. Meneja wa City, Pep Guardiola pia amethibitisha kipa Claudio Bravo anatarajiwa kukosa msimu wote uliosalia kufuatia majeruhi ya mguu aliyopata katika mchezo wa Manchester Derby. Aguero alipata majeruhi ya nyonga mwishoni mwa wiki iliyopita katika sare ya mabao 2-2 dhidi ya Middlesbrough, na ingawa vipimo vimeonyesha hakuumia sana lakini hatarajiwi kuwa fiti kwa ajili ya mchezo huo wa kesho. Akizungumza na wanahabari, Guardiola alithibitisha suala hilo na kuongeza kuwa Aguero anaweza kurejea uwanjani kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Leicester City.

No comments:

Post a Comment