Friday, May 12, 2017

ERIC BAILLY KUIKOSA FAINALI YA EUROPA LEAGUE.

BEKI wa Manchester United, Eric Bailly anatarajiwa kukosa mchezo wa fainali ya Europa League kufuatia kulimwa kadi nyekundu katika mchezo wa nusu fainali ya mkondo wa pili dhidi ya Celta Vigo jana usiku. Beki huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alitolewa kufuatia kumpiga usoni John Guidetti, huku Facundo Roncaglia naye pia akipata kadi nyekundu kutokana na tukio hilohilo. Hata hivyo, United hawakuadhibiwa huku Guidetti akikosa nafasi ya wazi dakika za mwisho ambayo ingeweza kuipeleka Celta Vigo katika hatua ya fainali. United sasa watavaana na Ajax Amsterdam ya Uholanzi katika hatua ya fainali itakayofanyika jijini Stockholm Mei 24 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment