Friday, May 12, 2017

AFUNGIWA MAISHA KUCHEZA KUFUATIA KUMPIGA MWENZAKE.MCHEZAJI wa soka la wanawake amefungiwa maisha kwa kumshambulia mpinzani wake ambapo picha zilimuonyesha akiwa amemkalia juu na kumpiga ngumi za uso. Mwanadada Silvija Sekacic alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo kati ya Zlejeznicar na Mladost, kufuatia kumkwatua Adnu Ljubanovic na kurudia kumpiga mara kadhaa mpaka walipotenganishwa. Sekacic hakuonyesha kujutia kitendo chake cha kutolewa nje hatua iliyopelekea kamati ya nidhamu ya Chama cha Soka cha Bosnia-Herzegovina kumfungia mwanadada maisha kucheza soka. Maafisa wa chama hicho wamesema kitendo kilichofanywa na Sekacic sio cha kisoka na hakikubaliki kamwe.

No comments:

Post a Comment