Friday, May 12, 2017

BOURNEMOUTH YAMTEMA WILSHERE.

MENEJA wa Bournemouth, Eddie Howe amesema anatafuta wachezaji wa kusjaili kwa ajili ya msimu ujao na hadhani kama itawezekana kumsajili moja kwa moja kiungo wa kimataifa wa Uingereza Jack Wilshere. Wilshere mwenye umri wa miaka 25 amekuwa kwa mkopo Bournemouth kwa msimu wote wakitokea Arsenal lakini amekosa mechi za mwisho wa msimu kufuatia kupata majeruhi ya mguu. Akizungumza na wahabari kuhusu mustakabali wa Wilshere, Howe amesema anadhani itakuwa ngumu kwao kumsajili kiungo huyo tena. Howe aliendelea kudai kuwa wanamtakia Wilshere kila la heri popote atakapokwenda msimu ujao. Wilshere aliumia katika mchezo dhidi ya Tottenham Hotspurs ambao walifungw amabao 4-0 Aprili 15 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment