Friday, May 12, 2017

KLOPP BADO ANA MATUMAINI NA TOP 4.

MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp ametania kuwa hahitaji dawa ili kuamini kuhusu nafasi ya kikosi chake kumaliza kwenye miongoni mwa timu nne za juu katika Ligi Kuu ya Uingereza. Matumaini ya Liverpool kujihakikishia nafasi ya kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao yaliingia dosari kufuatia sare ya bila kufungana na Southampton mwishoni mwa wiki iliyopita, mchezo ambao ulishuhudia James Milner akikosa penati kwenye kipindi cha pili. Liverpool bado wameendelea kubaki katika nafasi ya tatu lakini wamecheza mechi moja zaidi ya Manchester City na Arsenal ambao wako kwenye nafasi ya nne na tano. Akizungumza na wanahabari Klopp amesema kwa kawaida inapofika mwishoni mwa msimu shinikizo linakuwa kubwa hivyo suala hilo haliwezi kumnyima usingizi kwani bado anaamini wanaweza kumaliza kwenye nafasi nne za juu.

No comments:

Post a Comment