Friday, May 12, 2017

REDKNAPP AONGEZA MKATABA BIRMINGHAM.

MENEJA wa Birmingham City, Harry Redknapp amesaini mkataba mmoja zaidi wa kuendelea kuinoa klabu hiyo msimu ujao. Meneja huyo wa zamani wa West Ham United na Tottenham Hotspurs mwenye umri wa miaka 70 alichukua mikoba ya Gianfranco Zola kwenye klabu hiyo kwa ajili ya mechi tatu za mwisho kwenye Ligi ya Ubingwa. Redknapp amefanikiwa kuiokoa Birmingham isishuke daraja la kwanza kwa akushinda mechi mechi mbili kati ya tatu. Meneja huyo awali alipewa mkataba wa muda mfupi na kubainisha kuwa asingelipwa kama angeshindwa kuifanya Birmingham iepuke na balaa la kushuka daraja.

No comments:

Post a Comment