Friday, May 12, 2017

MAN UNITED KUPATA TIKETI KIDUCHU FAINALI YA EUROPA LEAGUE.

KLABU ya Manchester United inatarajiwa kupokea tiketi zisizozidi 9,500 kwa ajili ya fainali ya Europa League itakayofanyika katika Uwanja wa Friends Arena wenye uwezo wa kubeba mashabiki 50,000 uliopo jijini Stockholm. United watacheza na Ajax Amsterdam ya Uholanzi ambayo nayo itapata idadi kama hiyo ya tiketi kwa ajili ya mchezo huo wa Mei 24 mwaka huu.  Tiketi zote zilizosalia zitauzwa kwa jumla huku zikienda kwa waandaaji, vyama vya soka, wahisani kibiashara pamoja na wanahabari. Kwa mujibu ya ataaifa zilizotolewa na Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA zimedai kuwa kutakuwa hakuna sehemu jijini Stockholm itakayoonyeshwa mechi hiyo kwa ajili ya mashabiki watakaokuwa hawana tiketi.

No comments:

Post a Comment