Friday, May 12, 2017

BOATENG, SANCHEZ KUBAKIA BAYERN.

MENEJA wa Bayern Munich, Carlo Ancelotti amesisitiza Jerome Boateng na Renato Sanchez watabakia katika klabu hiyo msimu ujao pamoja na tetesi kuwa wawili hao wanaweza kutafuta changamoto mpya. Boateng amekuwa akipa majeruhi ya mara kwa mara msimu huu na kumfanya kufanikiwa kucheza mechi 11 pekee za Bundesliga. Taarifa kutoka nchini Ujerumani zilikuwa zikidai kuwa Boateng anataka kukutana na Bayern kujadili mustabali wake huku klabu za Ligi Kuu Tottenham Hotspurs na Arsenal zikitajwa kuwania saini yake. Lakini Ancelotti mwenye anetegemea Boateng atakabakia kwa ajili ya msimu ujao pamoja na kuwa na msimu mgumu kutokana na majeruhi ya mara kwa mara.
 Sanchez wakati anatua Allianz Arena akitokea Benfica alikuwa akitajwa kama mmoja wachezaji bora kabisa wanaochipukia kufuatia kiwango bora alichoonyesha katika michuano ya Ulaya akiwa na Ureno lakini mashabiki bado hawajaona ubora wa chipukizi huyo. Hata hivyo, Ancelotti amemkingia kifua akidai kuwa Sanchez huo ndio kwanza msimu wake wa kwanza na anaamini kutokana na uwezo alionao ataweza kung’aa kwenye timu hiyo kwa siku zijazo.

No comments:

Post a Comment