Tuesday, May 16, 2017

TERRY KUTUNDIKA DARUGA MWISHONI MWA MSIMU.

BEKI mkongwe wa Chelsea, John Terry bado hajaamua rasmi kama atastaafu soka kabisa ay la pindi atakapoondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu. Terry alianza kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa ligi toka Septemba mwaka jana, wakati mabingw ahao wapya waliposhinda mabao 4-3 dhidi ya Watford jana na kufanikiwa kufunga bao la kuongoza. Bao hilo linamfanya Terry kuwa mchezaji pekee kufunga bao katika kila msimu toka mwaka 2000 alipoibuka kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea. Akizungumza na wanahabari kuhusu mustakabali wake, Terry amesema hataki kuwa mchezaji ambaye anawazuia vijana chipukizi kupata nafasi lakini bado hajaamua kama mchezo dhidi ya Sunderland Jumapili hii utakuwa wa mwisho wake. Terry aliendelea kudai kuwa itategemea kama atapata ofa nzuri atakaa na familia na kuijadili kabla ya kufanya maamuzi.

No comments:

Post a Comment